Connect with us

Makala

Manula Awafunika Diarra,Mshery

Kipa wa klabu ya Simba sc Aishi Manula amewafunika makipa wa klabu ya Yanga sc Djigui Diarra na Aboutwalib Mshery baada ya kufanikiwa kucheza michezo 15 huku akitoka bila kufungwa(Clean Sheet) katika michezo tisa ya ligi kuu nchini.

Manula amekaa langoni kwenye mechi zote 15 ambazo Simba imecheza na amefungwa mabao 6 katika mechi hizo ambazo amekaa langoni huku akifuatiwa na Msheri ambaye amedaka michezo nane katika ya 15 bila kufungwa huku mingine akidakia katika klabu yake ya zamani ya Mtibwa Sugar.

Diarra ambaye nafasi yake ilishikiliwa na Mshery kipindi ambacho alikua yupo Afcon amepata Clean Sheet saba akiwa katika nafasi ya tatu huku Mussa Mbisa wa Coastal Union anashika nafasi ya nne kwa Clean Sheet akiwa nazo sita.

Makipa Ahmed Salula wa Azam FC inayotumia Uwanja wa Manungu Complex yeye ana clean sheet 5 sawa na Metacha Mnata wa Polisi Tanzania na James Ssetuba wa Biashara United ya Mara.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala