Connect with us

Makala

Karia Alia na Waamuzi

Rais wa shirikisho la soka nchini Wallace Karia amelalamika kuhusu ubora na ufanisi wa waamuzi katika mechi za ligi kuu nchini hususani zile zinazoihusisha Simba sc na Yanga sc kuwa na maamuzi tata yanayoleta maswali na migogoro kwa wadau wa soka nchini.

Karia amesema hayo wakati wa kufunga semina ya waamuzi wa ligi kuu iliyoandaliwa na shirikisho la soka nchini iliyofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam na kuhuduriwa na idadi kubwa ya waamuzi wa ligi kuu nchini.

“Waamuzi wanatakiwa walindwe, wasiingizwe katika matatizo ambayo sio ya kwao, hilo nitalisimamia nitahakikisha kwamba anayefuata kanuni tutaendelea kumlinda”
“Lakini wengine sio waaminifu, wamekuwa na matatizo mnatuharibia mchezo wetu kwa makusudi kabisa”
“Kuna maamuzi mmekuwa mkifanya mnatuletea tabu, nchi nzima taharuki hasa hizi timu zenu pendwa,, Maana na nyie mnazipenda pia lakini mko kazini”Alisema Karia
na kuhusu suala la kutumia teknolojia ya refarii wa njia ya Video Karia alikua na haya ya kusema “Watu wanasema sijui tutumie (VAR), mnajua gharama ?! Bahati nzuri Serikali inaliangalia hilo. Seti nzima ya (VAR) ni karibu Tsh 14.5 Bilioni nje ya Camera za Azam Tv”
“VAR wanatakiwa kuwa na Camera zao 📸 33 hadi 38 za aina tofauti,, Pia klabu zinapaswa ku-share Milioni 7 kila mechi”
Pia rais huyo wa Tff aligusia suala la wachambuzi wa soka nchini kuonekana wanashambulia upande mmoja “Kuna ninyi waandishi hasa nyie mnaojiita wachambuzi, mmekiwa mkiongeza taharuki sana wakati mwingine bila sababu, halafu lawama zote mnaleta kwangu”Alisema Karia
“Ukweli ni kwamba sijawahi kutoa maelekezo kwa waamuzi hata siku moja, ila nimekuwa muhanga wa matusi ya kila aina Naambiwa natoa maelekezo kwa waamuzi ili waamuzi wapendelee timu fulani” 🔍 Wallace Karia.
“Tunawaomba radhi wananchi wote, tunaahidi kutorejea makosa, tutafanya kazi kwa umakini mkubwa”

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala