Connect with us

Makala

Chanzo Ushindi wa Simba sc

Kikosi cha Simba sc juzi kilikua katika fomu ya juu kikiwafunga waivory Coast wa Asec Mimosa huku ikipiga mpira mkubwa na kufanikiwa kupata mabao 3-1 la wageni.

Awali mapema kabisa bilionea wa klabu hiyo ambaye kwa muda mrefu hakua nchini alirejea na moja kwa moja alikwenda kambini kufanya kikao na wachezaji huku wakilipwa stahiki zao zote pamoja na kuahidiwa kitita cha milioni 30 kwa kila mcheza endapo watashinda mechi zao tatu za kimataifa ambazo watacheza mwezi huu wa pili.

Inasemekana ujio huo wa nguvu wa bilionea huyo ambaye sio mchoyo wa kutoa fedha kwa mastaa wa klabu hiyo ndio siri ya mafanikio katika mchezo huo ambao Simba sc walipata bao la uongozi mapema tu kupitia kwa Pape Osmane Sakho aliyefunga kwa tiktaka dakika ya 12 akipokea pasi ya Shomari Kapombe aliyekua mwiba kwa wageni siku hiyo.

Pia ujio wa bosi umerejesha furaha na kujiamini kutokana na maneno ya faraja waliyopewa na bosi huyo kiasi cha nahodha John Bocco kuonyesha kiwango akichangia upatikanaji wa bao la tatu kwa pasi aliyompa Peter Banda dakika tatu baada ya Shomari Kapombe kufunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 78 bao ambalo lilisawazisha makosa ya beki Joash Onyango aliyewazawadia bao Asec Mimosa dakika ya 61.

Simba sc sasa itasafiri kwenda nchini Niger kuvaana na USGN iliyoanzishwa mwaka 1996 mchezo ambao utachezwa mwezi huu tarehe 20.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala