Connect with us

Makala

Yacouba,Kibwana Warejea

Wachezaji watatu wa klabu ya Yanga sc waliokua majeruhi wa muda mrefu Yacouba Sogne,Kibwana Shomari na Abdalah Shaibu wamerejea mazoezini baada ya kuwa majeruhi wa muda mrefu kikosini humo.

Miezi michache iliyopita wachezaji hao waliumia na kulazimika kupelekwa nchini Tunisia kwa ajili ya matibabu zaidi ya magoti ambapo walirejea nchini kuendelea na matibabu kisha wakarudi tena kwa matibabu ya mwisho nchini humo ambapo hivi sasa wapo tayari na wamekabidhiwa kwa mwalimu Nasredine Nabi kwa ajili ya kuwatumia.

Daktari wa Yanga sc Sheikh Mngazija amesema kuwa mastaa hao wameanza mazoezi ya nguvu tayari huku akiongezeka majeruhi mwingine ambaye ni Chrispin Ngushi japo hakubainisha tatizo halisi linalomkabili mshambuliaji huyo.

“Ngushi ishu yake ni tofauti na wengine baada ya kubaini tatizo lake imetulazimu kumpa mapumziko ya wiki sita, Nkane na Yassin ameanza mazoezi ya viungo wakati Yacouba, Kibwana na Ninja tayari wameanza mazoezi ya nguvu,” alisema Mngazija ambaye ni miongoni mwa madokta wazoefu.Alisema Daktari huyo mzoefu wa michezo nchini.

Yanga sc inakabiliwa na majeraha ya mara kwa mara ya mastaa wake ambao wamekua wakichezewa faulo za mara kwa mara na timu pinzani wanapokutana katika mechi za ligi kuu msimu huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala