Connect with us

Makala

Van De Beek Atua Everton

Kiungo wa klabu ya Manchester United Donny Van De Beek amejiunga na klabu ya Everton kwa mkopo wa miezi sita mpaka mwisho wa msimu ujao huku akikataa ofa za klabu za Valencia na Crystal Palace.

Kiungo huyo aliyejiunga na Man United akitokea Ajax Fc amekua chaguo la pili ama la tatu katika safu ya kiungo wa ushambuliaji klabuni Manchester huku Bruno Fernandes na Paul Pogba wakipewa kipaumbele katika eneo la ubunifu la juu la klabu hiyo.

Katika dili hilo klabu ya Everton italazimika kulipa mshahara wote wa kiungo huyo huku kukiwa hakuna kipengele cha kufanya uhamisho wa kudumu huku kiungo huyo akithibitisha kuwa fiti kwa mchezo ujao wa ligi kuu nchini humo dhidi ya matajiri wa Newcastle United.

Katika mahojiano yake kiungo huyo amesema kuwa amevutiwa kujiunga na klabu hiyo kutokana na ushawishi wa kocha mpya wa klabu hiyo Frank Lampard.”Nilikua na mazungumzo mazuri na kocha mpya,tulijadili kuhusu mpira na amenishawishi kujiunga na klabu hii” Alisema kiungo huyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala