Kutesa kwa zamu ndiyo msemo sahihi wa kuutumia kwa kipindi hiki wakati harakati za usajili ligi kuu bara zikiendelea kwa timu mbalimbali kujiimarisha hususani hizi za kariakoo,Iko hivi baada ya ripoti ya kocha mwinyi zahera kuwasilishwa kwa uongozi wa juu wa klabu ya Yanga,Jina la straika mrundi Amisi Tambwe limeorodheshwa kati ya mastaa wanaotemwa na kocha huyo baada ya kutoridhishwa na viwango vyao msimu uliopita ambapo yanga ilimaliza katika nafasi ya pili huku ikiwaacha watani zao simba wakitwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo.
Tambwe ambae amecheza ligi kuu kwa misimu sita mfululizo huku msimu wa kwanza akiutumia na simba sc kabla ya kutemwa na kuangukia jangwani ambapo amedumu kwa misimu mitano huku akifunga zaidi ya magoli 60 katika mashindano yote kuanzia desemba 2014,Huku ikiripotiwa kuporomoka kwa kiwango chake ndio sababu.
Kuporomoka kwa kiwango cha straika huyo mrundi kimesababishwa na majeruhi ya mara kwa mara hali iliyotoa nafasi kwa mkongo Haritier Ebenezer Makambo kuongoza safu ya ushambualiaji ya klabu hiyo na kufanya vyema hivyo hata Tambe alipopona alishindwa kushindana na kasi ya makambo aliyemaliza ligi na mabao 17 dhidi ya mabao nane ya Tambwe.
Mastaa wengine ambao wanatemwa na kocha mkongomani mwenye uraia wa ufaransa Mwinyi Zahera ni pamoja na Deus Kaseke,Said Juma “Makapu”,Mwinyi Haji Mngwali, Thabani Kamusoko,Klaus Kindoki,Jaffar Mohamed,Haruna Moshi na kipa Ibrahim Himid aliesajiliwa kutoka timu ya taifa ya soka la ufukweni.
Katika orodha hiyo baadhi ya mastaa wana mikataba na klabu hiyo hivyo watatolewa kwa mkopo kama mkongomani Klaus Kindoki huku wengine wakitemwa moja kwa moja.Sababu iliyotolewa kwa kutemwa kwa mastaa hao ni umri na viwango vyao kuwa chini hivyo hawana budi kuwapisha damu changa.
Mpaka sasa Yanga imekamilisha usajili wa mastaa saba wapya akiwemo kipa Metacha Mnata kutoka Azam Fc japo aliitumikia mbao kwa mkopo na huku taarifa zinadai bado inaendelea kuwafatilia saini za mastaa wengine watue klabuni hapo.