Connect with us

Makala

Mmeona Lakini,Ama Tuongeze Kidogo?

Ndio tambo za mashabiki wa klabu ya Simba sc baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Dar city kwa jumla ya mabao 6-0 katika mchezo wa upande mmoja uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaamm majira ya saa moja usiku.

Licha ya mchezo huo kutohudhuriwa na mashabiki wengi Simba sc waliingiza wachezaji wao wengi wa kikosi cha kwanza huku wakiwapumzisha Aishi Manula,Mohamed Hussein,Shomari Kapombe,Pape Osmane Sakho na sehemu kubwa ya mastaa wa eneo la kiungo pia wakipumzika na kumuachia dimba mkongwe Erasto Nyoni aliyetawala vyema eneo hilo.

Meddie Kagere alifungua kalamu ya mabao akifunga mara mbili dakika ya 5 na 13 huku Cletous Chama akifunga bao la tatu dakika ya 18 na dakika tatu baadae alimpasia Rally Bwalya aliyefunga bao la nne dakika ya 22 mabao yaliyodumu mpaka kipindi cha pili.

Pascal Wawa aliyeingia kuchukua nafasi ya Henock Inonga alifunga bao la tano kwa shuti dakika ya 48 ya mchezo na bao la mwisho likifungwa na Chris Mugalu ambaye alikosa takribani nafasi tatu za wazi kabla ya kufunga bao hilo zikiwa zimesalia dakika kumi mpira kuisha.

Licha juhudi za wachezaji wa klabu ya Simba sc kumsaidia nahodha John Bocco kufunga ili kuondoa ukame wa mabao lakini mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa na mwamuzi staa huyo alishindwa kufunga huku akikosa nafasi kadhaa za wazi ambapo klabu hiyo imefuzu hatua ya 16 bora na itakutana na Ruvu Shooting ambayo imewatoa Kmc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala