Connect with us

Makala

Azam Fc Yashusha Kocha Fundi

Klabu ya Azam Fc imeingia mkataba wa miaka mitatu na Omar Abdikarim Nasser kuwa Kocha Msaidizi mpya wa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Chamazi jijini Dar es salaam baada ya kukaa bila kocha msaidizi tangu iondoe benchi la ufundi chini ya George Lwandamina.

Ujio wa kocha huyo aliyesaini mkataba mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, ni sehemu ya mapendekezo ya Kocha Mkuu, Abdihamid Moallin ambaye tangu achukue nafasi kama kocha wa muda amefanikiwa kuibadilisha timu hiyo na kuanza kucheza soka linaloeleweka huku aitoa vipigo hasa kile cha bao 4 dhidi ya Prisons kiasi cha kuwafanya mabosi wa timu hiyo wampe mkataba mnono.

Nasser amewahi kufanya kazi katika nchi mbalimbali, mara ya mwisho 2019, akiitumikia moja ya vigogo vya nchini Qatar, Al Sadd, akiwa kama mchambuzi wa mechi (analyst) wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 23 (U-23), kabla ya kufanya majukumu kama hayo akiwa Al Duhail ya huko pia.

Al Sadd ni moja ya timu kubwa nchini humo, iliyokuwa ikinolewa na gwiji wa zamani wa Hispania, Xavi Hernandez, kabla kurejea Barcelona, akiwa kama Kocha Mkuu.

Mbali na kufanya kufanya kazi nje ya Taifa lake Somalia, pia alikuwa Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Somalia kuanzia mwaka jana hadi sasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala