Connect with us

Makala

Salah Aibeba Misri Dhidi ya Ivory Coast

Timu ya Taifa ya Misri imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-4 kwa penati dhidi ya Ivory Coast katika mchezo wa hatua ya mtoano kombe la mataifa ya Afrika nchini Cameroon.

mchezo huo ulimaliza dakika 120 bila bao ndipo ikafuata hatua ya changamoto ya mikwaju ya penati ili kupata mshindi wa kwenda hatua ya robo fainali kuungana na timu za Morroco,Senegal,Tunisia wenyeji Cameroon ambapo katika mikwaju 5 ya Ivory Coast walikosa mkwaju mmoja wa Eric Baily ambaye penati yake iliokolewa na kipa wa Misri.

Licha ya Wilfred Zaha kufunga mkwaju wa mwisho wa Ivory Coast lakini ufundi wa Mo salah uliwapeleka Misri hatua ya robo fainali baada ya kufunga mkwaju wa mwisho.

Sasa Misri inasubiri mshindi kati ya Mali na Equatorial Guinnea ili kujua nani ambaye itakabiliana nae katika hatua ya robo fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala