Connect with us

Makala

Kagera Sugar Yaifunga Simba sc

Klabu ya Simba sc imepoteza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar uliofanyika siku ya leo katika uwanja wa kaitaba baada ya kukubali kipigo cha 1-0.

Simba sc ilianza mchezo huo bila mshambuliaji halisi ambapo kocha Pablo Franco aliamua kuwatumia Bernad Morrison,Cletous Chama na Rally Bwalya katika safu ya ushambuliaji huku akiwaacha nje Chris Mugalu,Meddie Kagere na John Bocco mfumo ambao haukumpa matokeo licha ya mastaa hao kukosa nafasi kadhaa za kufunga.

Hamis Kiiza aliwanyanyua mashabiki wa Kagera Sugar dakika ya 71 baada ya timu hiyo kufanya shambulizi la kushtukiza baada ya Simba sc kupoteza mpira wakiwa wanalisakama lango la Kagera Sugar na ndipo zilipopigwa pasi tano za haraka haraka mpaka mpira kumkuta mfungaji aliyevunja mtego wa kuotea wa mabeki wa Simba sc.

Simba sc walijitahidi kutaka kurudisha bao hilo huku wakimtoa Benard Morrison na kumuingiza meddie Kagere lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Kagera sugar chini ya Nassor Kapama na Abdalah Mfuko kutokua na mafanikio.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala