Connect with us

Makala

Nigeria Yatolewa Afcon

Timu ya Taifa ya Nigeria imetolewa katika mashindano ya Afcon 2022 na timu ya taifa ya Tunisia baada ya kukubali kichapo cha 1-0 katika mchezo huo mkali na wa kusisimua uliofanyika Uwanja wa Roumdé Adjia Jijini Garoua,Cameroon yanapofanyika mashindano hayo makubwa barani Afrika.

Bao la Nahodha, Youssef Msakni dakika ya 47 limeipa Tunisia ushindi wa 1-0 dhidi ya Nigeria katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora na kuwaacha mashabiki wa Nigeria wakiwa hawaamini kilichotokea baada ya dakika 90 za mchezo kukamilika.

Awali Tunisia ilithibitisha kuwa mastaa saba wataukosa mchezo huo kutokana na kukutwa na Virusi vya Corona huku kocha wao Mondher Kebaier naye akikosa mchezo huo huku Nigeria wakiwa na rekodi nzuri ya ushindi wakiwa wameshinda mechi zote katika hatua ya makundi lakini bahati haikua upande wao baada ya kupoteza mchezo huo.

Ilikua ni siku mbaya kwa Alex Iwobi baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 67 ikiwa ni dakika saba tangu aingie uwanjani baada ya kucheza faulo mbaya iliyomlazimu refa kumpa kadi nyekundu hasa baada ya kuangalia picha za marejeo kupitia VAR na hali iliwalazimu Nigeria kucheza wakiwa pungufu kwa watu 10.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala