Connect with us

Soka

Nyoni,Abdulswamad watemwa Simba

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba sc imeweka wazi kuwaacha wachezaji wawili winga Duncan Nyoni kutoka Malawi na kiungo mkabaji Mtanzania Abdulswamad katika dirisha hili dogo la usajili.

Simba imechukua uamuzi huo kutokana na wachezaji hao kushindwa kulishawishi benchi la ufundi kuwapatia nafasi za kucheza kikosi cha kwanza.

Duncan alisajiliwa kama mchezaji wa kimataifa lengo likiwa ni kujaribu kuziba pengo liliachwa na Msumbiji Luiz Miquissone aliyetimkia Al Ahly ya Misri,hata hivo nafasi yake kikosini imekuwa ndoto kiasi cha kukosa kabisa kucheza,sawa na Abdulswamad aliyesajiliwa kuongeza nguvu eneo la kiungo wa chini lakini ameshindwa kufana hivyo.

Katika hatua nyingine klabu hiyo imemtoa kwa mkopo mlinda mlango namba tatu Jeremia Kisubi kwenda katika klabu ya Mtibwa sugar,huku ikwaleta nchini Shiboub,Moukoro na Udor kwaajili ya kufanya majaribio kupitia michuano inayoendelea ya Mapinduzi,na kuna uwezekano mkubwa mmoja wao kubakia kuchukua nafasi ya Nyoni.

Hata hivyo klabu hiyo inatajwa kuwa imemalizana na kiungo wake wa zamani Mzambia Clatous Chama kurejea katika klabu hio kwenye dirisha hili dogo la usajili.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka