Connect with us

Soka

Yanga sc Yamnyatia Nkane

Imeelezwa kwamba klabu ya Yanga sc imeanzisha mazungumzo na klabu ya Biashara United kuhusu kumsajili winga Dennis Nkane ambaye anahitajika klabuni hapo kwa mapendekezo ya kocha Nasredine Nabi ili kuimarisha winga zake klabuni hapo.

Yanga sc ipo katika mkakati mzito wa kuboresha kikosi chake ikiwa tayari inaelezwa kumalizana na Abubakary Salum kutoka Azam Fc kuja kumsaidia Feisal Salum eneo la kiungo wa juu huku pia ikiwa katika mkakati wa kuwaongezea mikataba mastaa wake ambao mikataba yao inaelekea mwishoni pia ikikataa kumuuza Saido Ntibanzokiza kwenda ulaya.

Nkane amekua ni mchezaji mwenye kasi na chenga za haraka ambazo zitaisaidia klabu ya Yanga sc kutokana na staili ya uchezaji ya klabu hiyo ya kushambulia kupitia pembeni ya uwanja eneo ambalo kwa sasa linatumika na Jesus Moloko na Farid Musa pekee kutokana na ufanisi wao.

Hata hivyo mchezaji huyo atakua na kazi ya kufanya ili kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kwani kuna mastaa wanakaa nje kutokana na changamoto ya namba akiwemo David Bryson na Dickson Ambundo ambao wamesajiliwa msimu huu.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka