Connect with us

Soka

Klopp kwenye kashfa na Waafrika

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ni kama ameingia kwenye mgogoro na Waafrika baada ya kuyaita mashindani ya mataifa Afrika ya soka(AFCON) kuwa ni mashindano madogo.

Klopp aliyasema hayo alipokuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya(Uefa champions league).

Katika mkutano huo Klopp alisema kuwa kuna mashindano madogo ya Afrika yanakuja mwezi Januari,kitu ambacho kilifanywa aulizwe na mmoja wa waandishi wa habari waliokuwepo kuwa kwanini ameyaita mashindano hayo kuwa ni madogo?

Kauli hiyo imepokelewa vibaya na wadau wa soka Afrika kwani kusema hivyo ni kudhalilisha mashindano hayo ambayo ni makubwa zaidi kwa Waafrika.

Hayo yamejiri kipindi ambacho Klopp ataenda kuwapoteza wacezaji wake Mane,Salah,Matip na Naby Keita kitu ambacho huenda kikawapunguzia kasi kwenye ligi kuu soka nchini Uingereza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka