Connect with us

Soka

Xavi amtaka tena Alcantara

Kocha mkuu mpya wa Barcelona Xavi Hernandes ameuambia uongozi wa timu hiyo kufanya linalowezekana kuhakikisha wanamrejesha nyumbani kiungo Thiago Alcantara anayekipiga ndani ya Liverpool.

Thiago aliondoka Cmp Nou mwaka 2014 na kutua Bayern Munich ya Ujerumani ambapo alicheza kwa mafanikio makubwa chini ya Pep Guardiola na kuwa mmoja wa viungo bora wa kati duniani.

Xavi anamhitaji mchezaji huyo aliyewahi kucheza nao ili kuongeza ubunifu na uongozi katikati ya uwanja eneo ambalo limepoteza ubora wake siku za hivi karibuni tofauti na miaka ya nyuma alipokuwa akicheza yeye na pacha wake Andres Iniesta.

Alcantara alijiunga na Liverpool 2020 akitokea Bayern Munich alikotwaa mataji kibao likiwamo la ligi ya mabingwa Ulaya msimu wa 2019/2020.

Hata hivyo haitakuwa rahisi kumpata fundi huyo mwenye miaka 30 kwani bado ana mkataba na Liverpool hadi mwaka 2024,hivyo Barcelona watapaswa kufungua pochi zao ili kumnasa.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka