Connect with us

Soka

XAVI KOCHA MPYA BARCA

Klabu ya soka ya Barcelona imemtangaza mchezaji na nahodha wao wa zamani Xavi Hernandes kuwa kocha mpya wa timu hiyo yenye makazi yake katika viunga vya Camp Nou Catuna Hispania.

Xavi atawasili nchini Hispania hii leo akitokea Qatar ili kusaini mkataba utakaomuweka hapo hadi mwaka 2024,pamoja na hilo atatambulishwa rasmi kwa wachezaji na wafanyakazi wa klabu hiyo.

Mkufunzi huyo aliwaaga wachezaji na wafanyakazi wa Al Sadd aliokuwa akifanya nao kazi katika klabu hiyo.

                                                         

Barcelona na Al Sadd walifikia makubaliano ya kuvunja mkataba wa kocha huo kwa thamani ya Euro milioni tano(5) ambazo zimelipwa na Xavi mwenyewe.

Xavi atatambulishwa rasmi mbele ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo siku ya Jumatatu katika dimba la Camp Nou.

Kocha huyo anafuata nyayo za wachezaji wa zamani wa timu hiyo ambayo walikuja kuwa makocha kama Pep Guardiola,Koeman na Ernesto.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka