Connect with us

Soka

REDONDO AITWA STARS

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Biashara United ya Mara Ramadhan Chombo ‘Redondo’ amitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ya mpira wa miguu Taifa Stars na kocha mkuu Kim Poulsen hii leo.

Ni miaka mingi tangu imepita kwa mchezaji huyo kuitumikia timu ya Taifa huku wadau wengi wa soka wakiamini hatorudi tena kikosini.

Chombo amewashangaza watu wengi kwa kiwango bora tangu ajiunge na Wanajeshi wa Mpakani Biashara united akiwa ni mmoja ya wachezaji waandamizi w=na muhimu mno kwenye kiosi hicho licha umri wake kuwa mkubwa.

Msimu huu mpaka sasa ameifungia Biashara magoli matatu(3) kwenye kombe la shirikisho la Afrika akitoa assisti moja huku akifunga mabao mengine mawili kwenye ligi kuu ya NBC katika michezo minne.

Baada ya kiwango chake kuwavutia wengi,wadau mbalimbali wa soka walianza kumpigia chapuo la kuitwa Taifa Stars ukizingatia upungufu wa viungo washambuliaji kwenye kikosi hicho.

Kocha wa Stars ameita kikosi cha wachezaji 27 kujiandaa na michezo miwili ya mwisho ya kundi J dhidi ya DR Congo na Madagascar kutafuta tiketi ya mtoano kufuzu kombe la dunia Qatar 2022.

Kikosi kamili;

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka