Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Manchester United ya nchinu Uingereza Ole Gunnar Solskjaer yupo hatarini kupoteza kibarua chake mara baada ya matokeo yasiyoridhisha ya timu hiyo siku za hivi karibuni.
Hilo limekuja mara baada ya Man Utd kupokea kipigo kizito na cha fedheha kutoka kwa wapinzani wakuu wa timu hiyo kwenye nchi hiyo Liverpool cha mabao 5-0 tena nyumbani Old Trafford.
Taarifa juu ya mustakabali wa kocha huyo zilianza kutoka Jumatatu asubuhi ambapo wachezaji na wafanyakazi wa viwanja vya mazoezi vya Carringhton hawakufika baada ya kuambiwa wabakie nyumbani tofauti na desturi ya timu hiyo kukutana kila Jumatatu asubuhi kwa ajili ya mazoezi ya kurejesha mwili baada ya mchezo wa wikiendi.
Mhariri wa gazeti la Manchenster Evening News Samuel Luckhurst anaeandika habari za Man Utd alilipoti kuwa Mtendaji wa klabu hiyo Richard Anold alifuta vikao vyote vya miadi ili afanye mazungumzo ya kina na mabosi wa timu hiyo familia ya Galzers juu ya mustakabali wa Solskjaer.
Katika hatua nyingine viongozi waandamizi wa klabu hiyo Alex Ferguson,Bobby Chalton na skauti mkuu wa timu hiyo pamoja na wamiliki Glazers walionkeana katika kitongoji cha Yorkshire kufanya kikao kizito juu ya mustakabali wa kocha wao.
Kocha wa zamani wa Juventus,Chelsea na Inter Milan Antonio Conte anapewa nafasi kubwa ya kuwa mkufunzi mpya wa klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford Jijini Manchester.