Connect with us

Soka

Ndayiragije aachishwa kibarua Geita Gold Fc

Baada ya kuanza ligi kwa kusuasua uongozi wa klabu ya Geita Gold Fc umefikia makubaliano ya pande zote mbili kusitisha mkataba na kocha wake mkuu Mrundi Etiene Ndayiragije hii leo.

Geita Gold haijaonja radha ya ushindi tangu ipande ligi kuu soka ya NBC msimu huu,wakipata alama mbili katika michezo minne ya ligi kuu.

Taarifa rasmi ya klabu imetolewa kupitia ukurasa rasmi wa instagram wa timu hiyo ukieleza kuwa timu hiyo sasa itakuwa chini ya kocha msaidizi Fred Minziro kwa muda mpaka watakapopata kocha mkuu mpya.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka