Connect with us

Soka

Mzambia atupia nne Europa league

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Zambia Patson Daka anayeichezea klabu ya Leicester city ya Uingereza ameifungia timu yake magoli manne(4) katika ushindi wa magoli 4-3 dhidi ya Sparta Praha katika ligi ya shirikisho Ulaya maarufu kama Europa league.

Daka aliyepata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwenye mchezo huo amefanikiwa kufunga mabao hayo dakika ya 45,48,54 na 79 na kuipatia timu yake ushindi ugenini.

Mshambuliaji huyo amejiunga na Leicester city katika dirisha lililopita akitokea klabu ya RB Salzburg ya Austria ambapo alikuwa na rekodi nzuri ya kufumania nyavu kwa mabingwa hao wa Bundesliga.

Uwezo mkubwa aliouonesha huenda ukamshawishi kocha mkuu wa kikosi hicho Brendan Rodgers kuanza kumtumia kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara japo ataumiza kichwa kutokana na viwango vya washambuliaji wengine Jamie Vardy na Kelechi Iheanacho kuwa vizuri kwa siku za hivi karibuni.

Wikiendi iliyopita mshambuliaji huyo alifunga bao lake la kwanza katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Man Utd kwenye ligi kuu nchini Uingereza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka