Connect with us

Soka

Ansu Fati asaini mkataba mpya Barca

Mshambuliaji kinda wa FC Barcelona Ansu Fati amesaini mkataba wa miaka sita kuendelea kukipiga katika viunga vya Nou Camp hadi mwaka 2027 huku kukiwa na kipengele cha kumsajili chenye thamani ya Euro bilioni moja.

Huo ni muendelezo wa klabu hiyo kuendelea kuwatia vitanzi wachezaji wao makinda baada ya awali kumsainisha Pedri mkataba mpya,hali hiyo ni kama tahadhari ya kuhofia kuwapoteza hasa kipindi hiki timu hiyo ikipitia ukata mkubwa katika historia ya klabu hiyo.

Taarifa rasmi ya klabu ya twitter imethibitisha hilo

Barca wapo kwenye mazungumzo na wachezaji wengine makinda Pablo Gavira,Oscar Mingueza na Ronald Araujo kuwaongezea mikatabu mipya.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka