Connect with us

Soka

Ansu Fati mbioni kujitia kitanzi Barca

Mshambuliaji kinda wa FC Barcelona Ansu Fati anatarajiwa kutia saini makubaliano ya mkataba mpya kati yake na klabu yake hivi karibuni mara baada ya mzungumzo ya pande mbili kwenda vizuri.

Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona Ramon Planes alilazimika kusafiri hadi nchini Ureno kukutana na wakala wa mchezaji huyo Jorge Mendes juu ya kuongeza mkataba mpya kwa Fati.

Hapo awali iliripotiwa kuwa Mendes hataki mchezaji wake huyo awekewe kipengele cha kuuzwa chenye thamani ya Euro milini 850 hali ambayo ilizua wasiwasi juu ya hatma ya mshambuliaji huyo,hata hivyo bado haijajulikana kama amekubali hilo au laa.

Barcelona inamuona Ansu Fati kama sura na mchezaji wa kutumaini wa klabu hiyo na kwa kulithibitisha hilo walimpatia jezi namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na gwiji wa timu hiyo Lionel Messi aliyetimkia PSG.

Klabu hiyo ipo pia kwenye mipango ya kuwaongezea mikataba mipya wachezaji wengine makinda Gavira,Araujo na Oscar Mingueza wakikamilisha dili la Ansu Fati.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka