Connect with us

Soka

Yanga yapaa kileleni NPL

Mabingwa wa kihistoria nchini Yanga Sc imekwea kileleni mwa msimamo ligi kuu ya NBC baada ya ushindi wa mabo 2-0 dhidi ya watoza ushuru wa Manispaa ya Kinondoni KMC katika mchezo uliofanyika katika dimba la Majimaji Songea.

Yanga walijipatia goli la kwanza dakika ya 6 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji wake Fiston Mayele akimalizia shuti la Fei Toto,kabla ya kiungo fundi Feisal Salum kuhitimisha kalamu hiyo kwa mkwaju mkali wa nje ya box dakika ya 12 na kuamsha shangwe kwa mashabiki.

                                                     

Kipindi cha pili KMC waliamka na kujaribu kusawazisha magoli hayo kwa kucheza soka safi lakini hawakufanikiwa kutokana na safu ngumu ya ulinzi ya Yanga.

Wananchi hao sasa wanaoongoza msimamo huo katika raundi hii ya tatu huku wapinzani wake Simba wakisubiri kiporo chao tarehe 27 Oktoba dhidi ya Polisi Tanzania.

Yanga watarejea Dar es salaam kujiandaa na maandalizi ya mchezo wao mwingine mkali dhidi ya waoka mikate Azam Fc ambao watashuka dimbani usiku huu kuwakabili wauwaji wa kusini Namungo Fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka