Connect with us

Soka

Kocha Yanga alia na TFF kisa Maproo

Kocha mkuu wa kikosi cha Yanga Mtunisia Nasreedin Nabi amelilamikia shirikisho la mpira wa miguu nchini(TFF) juu ya kanuni ya kusimamia idadi ya wachezaji wa kimataifa wanaoruhusiwa kuwa kwenye kikosi cha mechi katika michezo ya ligi kuu soka Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa kanuni za ligi timu inayoshiriki ligi kuu itaruhusiwa kutumia wachezaji nane tu wa kigeni katika mchezo wa ligi kati ya kumi na mbili wanaoruhusiwa kusajiliwa.

Kwa mantiki hiyo Yanga yenye wachezaji kumi wa kigeni italazimika kutowatumia wachezaji wawili kwenye kila mchezo wa ligi hali inayozua tafrani kwenye kikosi na benchi la ufundi.

Katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa ligi dhidi ya KMC huko Songea,Kocha Nabi amesema hali hiyo inamchanganya katika maandalizi lakini ni hasara kwa klabu kwani zinatumia kiasi kikubwa kuwahudumia wachezaji hao na hawachezi.

Aliendelea kwa kusema kuwa kanuni imeleta shida kwani imekuja baada ya dirisha kufungwa,wao kama Yanga wangejua hilo mapema wasingesajili wachezaji kumi wa kigeni.

Kipindi cha hivi karibuni kocha huyo inasemekana aliingia kwenye mgogoro na nyota wa Burundi Ntibanzokiza kisa kikitajwa ni kutojumuishwa kwenye kikosi mara kwa mara na hata kwenye mchezo wa kesho wa ligi kuu hajajumuishwa sababu ikitajwa ni idadi ya wachezaji wa kigeni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka