Connect with us

Soka

CAS yapeleka tena mbele kesi ya Morrison

Mahakamma ya usuluhishi wa michezo duniani (CAS) imesogeza kesi ya kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji wa Simba SC Benard Morrison kutoka leo Septemba 21 hadi Oktoba 26 mwaka huu.

Morrison anatuhumiwa na Yanga SC kujiunga kwa watani wao wa jadi Simba SC wakati akiwa bado ana mkataba na mabingwa hao wa kihstoria.

Awali kesi yake ilitarajiwa kuwa ingetolewa maamuzi baada ya kusikilizwa na CAS kwa njia ya video Julai mwaka huu na hukumu yake wakisema ingetolewa kufikia August 24.Ilipofika August 24 CAS waliomba radhi kwa Yanga na Morrison kuwa walijisahau hivyo watalishughulikia swala hilo na kutoa hukumu Septemba 21 mwaka huu.

Wadau na wapenzi wa soka walikua wakisubiria hukumu ya kesi hiyo kwa hamu siku ya leo kabla ya CAS kupitia tovuti yake kueleza kuwa hukumu ya kesi hiyo imesogezwa hadi Oktoba 26 mwaka huu.

Morrison alishinda kesi hiyo hapa nchini kupitia kamati ya hadhi na maadilim ya wachezaji ya TFF lakini Yanga SC hawakuridhika na kuamua kukata rufaa CAS ambapo kesi imeshasikilizwa kilichobaki ni hukumu tu kujua mbivu na mbichi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka