Connect with us

Soka

Man Utd,Chelsea zaikaba koo Liverpool kileleni EPL

Vilabu vya Manchester United na Chelesea vimeshinda michezo yao ya leo ya ligi kuu soka nchini Uingereza  na kuendelea kufungana alama na vinara wa ligi hiyo klabu ya soka ya Liverpool.

Manchester United wamepata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya West Ham katika dimba la London.Wst Ham ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 30 kabla ya Ronaldo kuisawazishia United dakika ya 35 akiunganisha krosi ya Bruno Fernandes.Jesse Lingard aliipatia tgoli la ushindi dakika ya 89 kwa shuti lililotinga nyavu za juu.

West Ham walipta nafasi ya kusawazisha dakika ya 90+3 baada ya Shaw kuunawa mpira na kuamuliwa penati,ambayo De gea aliikoa na kuisaidia timu yake kuondoka na alama zote tatu.Katika mchezo mchezo huo

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo Chelsea wameibuka na ushindi wa magoli 3-0 didi ya Tottenham

Hotspurs katika dimba la dimba Tottenham Hotspurs.Mashujaa wa Chelsea walikua ni  Thiago Silva

aliyefunga kwa kichwa dakika ya 49 kabla ya kuongeza la pili dakika ya 57.Antonio Rudiger alihitimisha ushindi huo kwa kutupia goli la tatu dakika ya 92.

 

 

 

Kwa matokeo hayo timu zote tatu za Chelsea,Man Utd na Liverpool zimelingana alama zikiwa na 13 kila mmoja huku Chelsea akikaa kileleni kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa baada ya michezo mitano.msimamo wa ligi hiyo kwasasa ni kama ifuatavyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka