Connect with us

Soka

Yanga SC yamtambulisha Bangala

Klabu ya soka ya Yanga imemtambulisha beki kisiki raia wa Jmhuri ya Kidemokrasia ya Congo Yannick Bangala Litombo kukipiga Jangwani katika kambi yao huko Marakesh Morocco.

Bangala amesaini kandarasi ya miaka miwili kuwatumikia Wanachi na tayari amejiunga na wenzake kwenye maandalizi ya msimu nmpya yanayoendelea huko Morocco.

Beki huyo amewahi kuitumikia AS Vita ya Congo kama nahodha kabla ya kwenda FAR Rabat ya Morocco na amekuwa akiitwa mara kadhaa kuitumikia timu ya Taifa ya DRC.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka