Connect with us

Makala

JKT Washindwa Mziki Wa Simba

Simba Sc imewapa kichapo cha mabao 4-0 JKT Tanzania katika mchezo wa raundi ya tano ya ligi kuu bara uliochezwa jana uwanja wa Jamuhuri mkoani Dodoma majira ya Saa 8:00mchana.

Meddie Kagere alipachika mabao mawili dakika ya 3′ na 41 huku Chris Mugalu naye hakuwa nyuma katika kipindi cha kwanza cha mchezo ambapo alicheka na nyavu dakika ya 6.

Bao lililokosha mashabiki wa Simba Sc na wakainuka wote uwanjani ni lile ambao lilipachikwa dakika ya 54 na Luis Miquissone ambapo lilidumu hadi dakika 90 za mchezo na kuwafanya wekundu hao kuondoka na alama tatu muhimu.

Aishi Manula alikuwa na jitihada kubwa sana za kulinda lango la Simba Sc licha ya Mashambulizi kuwa mengi hakuruhusu bao lolote.

Katika msimamo wa ligi kuu Simba ipo nafasi ya 2 ikiwa imejikusanyia pointi 13 katika raundi ya 5 ya ligi kuu huku vinara wakiwa Azam Fc wenye pointi 15.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala