Connect with us

Makala

Pluijm Yupo Tayari Kurejea Yanga

Kocha wa zamani wa Yanga ambaye ni Mholanzi, Hans Pluijm amefungukia hatma yake ya kurejea na kukinoa kikosi hicho kwa mara ya tatu baada ya tetesi nyingi kuzagaa kuwa jina lake litajwe kwenye orodha ya makocha wanaowaniwa na Yanga ,hii ni baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mbelgiji Luc Eymael kufutwa kazi.
Pluijm amesema kuwa bado viongozi wa Yanga hawajamfuata kwa ajili ya kufanya mazungumzo lakini yupo tayari kurejea kukinoa kikosi hicho kwani hana timu yoyote anayoifundisha kwa sasa na uzuri ni kuwa anawafahamu wachezaji baadhi wa Yanga na alishafanya nao kazi hivyo hatakuwa na kazi kubwa.

Jina jingine la kocha  linalotajwa kwenye orodha ya makocha wanaotarajiwa kujiunga na Yanga katika msimu ujao ni Ernie Brandts raia wa Uholanzi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala