Connect with us

Soka

Kakolanya Akinukisha Simba sc

Golikipa namba mbili wa klabu ya Simba, Beno Kakolanya amemshangaa kocha wa makipa wa klabu hiyo Mohamed Mwarami kwa kumsema hayupo fiti kwa kocha mkuu wa Simba (Sven) na hawezi kucheza na mechi ya ushindani.

Beno tangu likizo ya Corona ameshindwa kucheza na hata kukaa benchi kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania kwa madai ya kuwa hayupo fiti kitu ambacho golikipa huyo amekipinga waziwazi na kusema kocha huyo anamchukia tu.

Baada ya mkanganyiko huo jana Kakolanya alimshitaki kocha wa makipa (Mwarami) kwa makocha wa Simba kwa kumsingizia anaumwa (hayupo fiti) wakati hata haumwi na hajawahi kukosa program yeyote ya timu tangu irejee baada ya Corona.

Credit:Yossima Sitta jr

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka