Connect with us

Soka

Yanga Yamalizana na Kotei

Imeripotiwa kuwa klabu ya Yanga ya Tanzania wamekamilisha dili la kumsaini kiungo wa Ghana James Kotei,
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 aliandika makubaliano na klabu hiyo (Yanga) baada ya mazungumzo ya mafanikio .

Kotei anarudi Afrika Mashariki baada ya kandarasi yake kusitishwa kwa makubaliano binafasi baina ya mchezaji mwenyewe na Klabu yake aliyokuwa akikipiga huko Belarusi ya FC Slavia Moyzr kwani hakufanikiwa hata kumaliza msimu moja kutokana na kuandamwa na majeraha .

Kiungo huyo wa zamani wa Simba Sc anatarajiwa kuvalia jezi za njano na Kijani katika siku zijazo baada ya
Aliiachana na klabu ya Simba SC mnamo 2019 kufuatia kumalizika kwa mkataba wake klabuni hapo .

Alisaidia Simba SC kushinda Ligi Kuu ya Tanzania mara mbili na kufuzu kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa CAF ya 2018/19 .

Kotei alijiunga na Kaizer Chiefs huko Afrika Kusini lakini aliondoka baada ya muda wa miezi 6 tu baada ya kushindwa kuonesha cheche zake na miamba hao wa South chini ya Kocha mkuu bwana Ernst Middendorp .

Cc:Dominick Salamba

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka