Connect with us

Soka

Yanga Yatua Bungeni

Klabu ya Yanga mapema leo asubuhi iliwasili katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma baada ya kupata mwaliko.

Timu hiyo iliwasili ikiwa imeambatana na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM injinia Hersi Said pamoja na viongozi wengine wa klabu hiyo huku wakilakiwa na Waziri wa Habari na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe.

Klabu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1935 ni mabingwa wa kihistoria nchini wakiwa wametwaa taji la ligi kuu mara 27 wapo jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Jkt Tanzania siku ya Jumatano.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka