Connect with us

Soka

Mo Afungukia Usajili Simba sc

Bilionea wa klabu ya Simba sc Mohamed Dewji amewataka wanasimba kuwa watulivu hasa katika kipindi hiki cha usajili kwani watasajili mchezaji yeyote wanayemtaka.

Mo amesema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter ambapo alisema mashabiki hao hawana haja ya kuhofia chochote kwani watasajili mchezaji yeyote atakayependekezwa na mwalimu kutoka timu yeyote.

“Wanasimba wenzangu nataka niwahakikishie hakuna mchezaji yeyote atakayeondoka Simba lakini pia tutasajili mchezaji yeyote kutoka mahali popote kama mwalimu wetu atamhitaji,Tutashuka kwa kishindo hatuna maneno mengi lakini tupo”.

Kauli hiyo inaweza kuwa mwiba kwa wapinzani wao Yanga sc ambao wanashindani kuwasajili mastaa kadhaa akiwemp Bakari Mwamnyeto na mastaa wa kigeni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka