Connect with us

Soka

Straika Rasta Kutua Yanga

Alfred Raul ambaye ni wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa Burkina Faso, Yacouba Sogne amethibitisha kuwa Nyota huyo wa zamani wa Asante Kotoko ya Ghana atajiunga na Klabu ya Yanga SC ifikapo mwisho wa msimu huu.

Wakala huyo anayeishi nchini Ufaransa amesema tayari mazungumzo yalishafanyika na nyota huyo alishakubali kutua Yanga kinachosubili tu ni mipaka ya Burkina Faso ifunguliwe ili aweze kuja nchini kusaini mkataba.

Hata hivyo kocha wa zamani wa klabu ya Yanga Hans Van De Plujm amesema staa huyo ni mchezaji mzuri japo thamani yake halisi sio hiyo inayotajwa kwani inakuzwa na mitandao na ana uwezo wa kuitafutia klabu hiyo mastaa wa maana kwa bei chee.

Yanga imekua ikihangaika kupata mshambuliaji baada ya waliokuwapo kushindwa kuendana na kasi ya timu hiyo na hivyo kuna uwezekano mkubwa watatemwa muda wowote.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka