Connect with us

Makala

Ajibu Aruhusiwa Kusepa Mazima Simba

Uongozi wa Simba wamemruhusu kiungo wao, Ibrahim Ajibu kuondoka muda wowote atakaohitaji na kwenda kujiunga na klabu yoyote itakayomuhitaji baada ya uongozi huo kupata taarifa zilizozagaa kuwa mchezaji huyo anataka kuondoka kwenye kikosi hicho ili kujiunga na timu moja ya nje ya nchi.
Ajibu alijiunga na Simba msimu huu kwa dau la Sh Mil 80 akitokea Yanga mara baada ya mkataba wake wa miaka miwili kumalizika ila inaelezwa kuwa timu hiyo imemruhusu kiungo huyo kuondoka lakini lazima masharti maalum yafuatwe.
Wakati kiungo huyo anasajiliwa Simba akitokea Yanga, mabosi walikuwa wana matarajio makubwa ya kumuona Ajibu akicheza kwa mafanikio katika msimu huu lakini imekuwa tofauti na matarajio yao hivyo uongozi umekubali kuachana naye kwani hayupo kwenye mipango ya kocha kuelekea msimu ujao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala