Connect with us

Soka

Bundasliga Kurudi May 16

Ligi kuu nchini Ujerumani inatarajiwa kurejea mnamo May 16 baada ya timu zote 36 za madaraja ya juu kukubaliana ili msimu uishe June 30.

Ligi hiyo inarejea baada ya Kansela wa nchi hiyo Angel Merkel kuruhusu shughuli zirejee kufuatia kufungwa ili kupisha maambukizi ya Virusi vya ugonjwa wa Corona uliokua umeingia kwa kasi nchini hadi kupelekea ligi kuu na ligi za madaraja ya chini kusimamishwa machi.

Licha ya kuruhusiwa kuendelea kwa ligi hiyo,bado itachezwa bila mashabiki kufuatia katazo la serikali kuhusu kutokua na mkusanyiko wa watu wengi mpaka mwezi Agosti mwaka huu.

Moja ya kivutio kikubwa katika siku hiyo ya kurejea kwa ligi ni mechi ya mahasimu baina ya Borrusia Dortmund na Schalke 04 huku Bayern Munchen wakiwavaa Union Berlin na watu wengi watasubiri pambano kati ya Bayern na Dortmund litakalopigwa kati ya mei 26 au 27.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka