Connect with us

Makala

Bigirimana Blaise-Nitaingia Yanga Kwa Utaratibu

Raia wa Burundi anayekipiga ndani ya Namungo FC ,Bigirimana Blaise amesema kuwa hana hiyana ya kutua ndani ya kikosi cha Yanga iwapo watafuata taratibu za usajili.

Blaise kabla ya msimu kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona alikuwa mchezaji mzuri wa  kucheka na nyavu ambapo  ametupia jumla ya mabao 10 kati ya 34 yalifungwa na klabu yake.

Nyota huyo alisema kuwa awali viongozi wa Yanga waliwahi kumfuata ili wapate saini yake ila walighairi baada ya kuona mambo hayajaenda sawa na tayari alishatua Namungo.

“Bado nina mkataba na Namungo ambao utaisha pindi msimu ukiisha iwapo watakuja na tukafikiana makubaliano sina hiyana nipo tayari kuvaa jezi ya Yanga, sichagui hata ikitokea ni Kagera Sugar ama Simba kikubwa maelewano na utaratibu ufuatwe,” alisema Blaise

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala