Connect with us

Soka

Mabeki Simba Sc Kikaangoni

Klabu ya Simba sc ina mmpango wa kusajili mabeki wapya watatu baada ya  waliokuwepo klabuni hapo kutokua na viwango vya kuridhisha kwa mujibu wa benchi la ufundi la klabu hiyo.

Taarifa kutoka nadni ya klabu hiyo zinadai kwamba kocha Sven Vandebroek haridhishwi na viwango vya baadhi ya mabeki wa klabu hiyo hasa Yussuph Mlipili na Tairone Dos Santos huku Pascal Wawa na Erasto Nyoni wakiwa na umri mkubwa hivyo kushindwa kuhimili mikiki ya vijana.

Kufuatia hali hiyo inadaiwa tayari uongozi wa klabu hiyo umewapa kazi mawakala mbalimbali barani Afrika kusaka wachezaji haon ili iwanase mapema kuelekea michuano ya kimataifa na idadi ya mabeki wanaowindwa na klabu hiyo ni watatu wa kati ambapo mmoja anatakiwa awe na uwezo wa kucheza pembeni.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka