Connect with us

Soka

Simba Yamalizia Hasira Kwa Singida Utd

Klabu ya soka ya Simba sc imeifunga timu ya Singida United mabao 8-0 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Simba ilipata bao la mapema dakika ya 2 ya mchezo kupitia kwa Meddie Kagere aliyefunga mengine dakika za 26,42 na 71 huku pia Deo Kanda akifunga mabao mawili dakika za 13 na 19 na John boko akifunga bao moja dakika ya 20 na Sharaff Eldin Shiboub akifunga pia dakika ya 60.

Simba imeendelea kujikita kileleni mwa ligi kuu huku ikiwa na dalili zote za kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo huku Singida United ikizidi kudidimia na ikionyesha dalili zote za kushuka daraja.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka