Connect with us

Soka

Corona Yasimamisha Serie A

Waziri mkuu wa Italia Guissepe Conte amesema michezo yote ya ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A itasimama mpaka April 3 ili kupisha maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Corona ulioingia nchini humo.

Waziri huyo amefikia maamuzi hayo baada ya takribani watu 450 kuripotiwa kupoteza maisha huku zaidi ya watu 9000 inakadiliwa wameambukizwa ugonjwa huo unaoenezwa kwa njia yan hewa na majimaji ya mwilini.

Awali serikali nchini Italia ilizuia mikusanyiko ya watu ikiwemo kuamuru mechi za ligi zichezwe bila mashabiki ikiwemo mechi iliyochezwa wiki iliyoisha baina ya Intermilan dhidi ya Juventus ambapo hakukua na mashabiki walioingia uwanjani.

Licha ya kusimamishwa kwa ligi hiyo,michuano ya kimataifa ikiwemo klabu bingwa barani ulaya na ligi ya kombe la Europa itaendelea kama kawaida bila mashabiki.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka