Connect with us

Soka

Yanga Saresare Maua

Ni sare ya nne mfululizo kwa klabu ya Yanga sc baada ya jana kutoka sare na timu ya Coastal union katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Awali Yanga ilitoka sare ya 1-1 na Mbeya city kisha dhidi ya Prisons Fc na ikasafiri kuifuata Polisi Tanzania napo ikatoka sare ya 1-1 na jana pia ikapata matokeo ya bila kufungana na wagosi wa kaya.

Yanga imeambulia pointi 4 kati ya 12 katika michezo minne na itahitaji kushinda mechi zake 16 zilizosalia huku ikiwaombea Simba sc wapoteze mechi 6 kati ya 14 walizobakisha ili wawe mabingwa.

Mpaka sasa Simba ipo kileleni ikiwa na pointi 62 huku Yanga ikiwa nafasi ya nne na pointi 41 baada ya kucheza mechi za wikiendi hii japo ina michezo miwili mkononi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka