Connect with us

Soka

Yanga Ndo Basi Tena

Yanga imejitoa rasmi katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kukubali sare ya tatu mfululizo mbele ya Polisi Tanzania katika mchezo uliofanyika mjini Moshi katika uwanja wa Ushirika.

Yanga ilitangulia kupata bao dakika ya 41 kupitia kwa Tariq Seif aliyeunganisha kwa kichwa pasi ya Benard Morrison kufuatia uzembe wa mabeki wa Polisi bao lililodumu mpaka mapumziko.

Polisi walisawazisha bao hilo kwa kichwa kufuatia kona ya Marcel Kaheza iliyomkuta mfungaji Sixtus Sabilo aliyepiga kichwa akiwa hajakabwa.

Yanga imeendelea kubaki nafasi ya tatu huku ikiachwa pointi 11 na vinara simba sc ambao wanashuka dimbani jioni hii kuikabili Ndanda fc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka