Connect with us

Soka

“Nitaendelea Kufungwa Tu”-Manula

Kipa wa timu ya Simba sc Aishi Manula amesisitiza kuwa ataendelea kufungwa endapo atakaa langoni kuidakia timu hiyo katika michezo mbalimbali.

Manula alibainisha hayo wakati akimjibu shabiki mmoja katika mtandao wa instagram baada ya shabiki huyo anayetumia jina la Oscarlameck3420 kumtaka kipa huyo kuwa siriazi na kazi pia apunguze makosa madogo madogo.

Ujumbe huo ulionekana kumkera kipa huyo na ndipo alipoamua kujibu kuwa ataendelea kufungwa tu.

“Nitaendelea kufungwa kwa vyovyote vile iwe mbali au karibu,Iwe pembeni ama kati njia pekee ya mimi kutofungwa na kukaa benchi tu.Aliandika kipa huyo

Manula amekua na misukosuko baada ya kufungwa bao na Balama Mapinduzi katika mchezo wa watani wa jadi hali iliyosababisha awekwe benchi huku nafasi yake ikichukuliwa na Benno Kakolanya japo jana alicheza dhidi ya mtibwa na kufanya vizuri.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka