Connect with us

Soka

Yanga Yapoteza Pointi

Klabu ya Yanga imeshindwa kuendelea kupunguza pengo la pointi dhidi ya mahasimu wao Simba baada ya kukubali sare ya 1-1 dhidi ya Mbeya city katika mchezo uliofanyika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Mbeya city walliokuwa wakicheza kwa mkakati maalumu wa kutofunguka walifanikiwa kupata bao dakika ya 42 baada ya beki Lamine Moro kujifunga katika harakati za kuokoa mpira.

Morrison aliendelea kuwa shujaa wa Yanga baada ya kufunga bao la kusawazisha dakika ya 75 na kufanikiwa kurejesha pointi moja iliwafanya kufikisha pointi 38.

Yanga inakumbukumbu ya kushinda bao 1-0 mbele ya Ruvu Shooting na Mbeya City ilishinda bao 1-0 mbele ya Tanzania Prisons.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka