Connect with us

Makala

Serikali Yawataka Makocha Wapya Kulipa Kodi

Serikali imezitaka timu za mpira zilizoajiri makocha na wachezaji kutoka nje ya nchi kutoa taarifa kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ya waajiriwa walionao ili kulipa kodi.
Naibu wa Waziri wa fedha na mipango Mhe.Daktari Ashatu  Kijaji amezungumza alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Chemba Juma Selemani Nkamia Jijijini Dodoma, aliyetaka kujua Serikali inatambuaje kocha au mchezaji wa nje aliyelipa na asiyelipa kodi.
“Kila mgeni akifikisha miezi 6 anahesabika ni mkazi (local resident) na anapaswa kulipa kodi na jukumu la mwajiri kutoa taarifa ya nani analipwa nini ili kodi zote stahili ziweze kulipwa kwa mujibu wa sheria” alieleza Dkt. Kijaji.
Aliongeza kwa kusema kuwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya Sh. milioni 1,733.6 zilikusanywa kama malipo ya kodi ya ajira kutoka kwa makocha na wachezaji wa kigeni wanaofanya kazi hapa nchini.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala