Connect with us

Makala

Juventus Kumng’oa Mmoja Liverpool

Taarifa inayosambaa kwa kasi ni kwamba Juventus imejipanga kumng’oa beki wa Liverpool Virgil van Dijk katika usajili wa dirisha lijalo la majira ya joto barani Ulaya.

Gazeti la The Sun la Uingereza jana limeeleza kuwa Juventus imemtengea beki huyo donge nono la pauni milioni 150 ambayo ni sawa na Sh bilioni 456.

Miamba hiyo ya serie A inaamini kuwa mholanzi huyo atatafuta changamoto mpya kama timu yake ikibeba ubingwa wa premier msimu huu na wanataka kumfanya awe beki ghali zaidi duniani kwa mara nyingine tena.

Van Dijk ameisaidia Liverpool kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Dunia la Klabu na Uefa Super Cup huku wakiwa mbioni kubeba ubingwa wa kwanza wa Premier baada ya kupita miaka 30 tangu alipotua Anfield.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala