Connect with us

Makala

Mzungu Yanga Atoa Tamko

Mambo ni moto katika uongozi wa Yanga kwenye harakati za kutaka kubadilisha mfumo wa uendeshwaji kwenda kibiashara zaidi.

Uongozi huo ulimshusha juzi nchini Cerraca Antonio Pinto kutoka Ureno kwa ajili ya kuja kusimamia mchakato wa mabadiliko kwani amewahi kuwa mtendaji mkuu wa vigogo wa Ureno Benfica.

Pinto baada ya kutua nchini alimshukuru Mungu kwa kufika salama nchini na alichoweza kuwaambia Wanayanga ni kwamba wategemee kupata mambo mengi ambayo yataifanya klabu yao kuwa moja kati ya klabu kubwa Afrika.

“Nitahakikisha nafanya kazi iliyonileta kwa umakini mkubwa na ni matumaini yangu kila kitu kitakuwa sawa na kuifanya iweze kujiendesha kibiashara katika soka la kimataifa,” alisema Pinto

Pinto anatarajiwa kukutana na uongozi wa klabu hiyo leo na kufanya kikao maalam kabla ya kuanza kuifanya kazi yake iliyomleta klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala