Connect with us

Soka

Lamine Arejea Yanga

Wakati ikiivaa Jkt Tanzania leo klabu ya Yanga imepata ahueni baada ya beki raia wa Ghana Lamine Moro kurejea baada ya kuwa majeruhi kwa wiki kadhaa.

Lamine aliumia wakati wa mechi ya kimataifa dhidi ya Zesco ugenini nchini Zambia na tangu hapo amekua na hali isiyotengemaa hivyo kukosa michezo kadhaa ya ligi kuu na ya kimataifa huku pia akiwa na kadi mbili za  njano ambayo ilimfanya ashindwe kucheza michuano ya Caf.

Lamine amerejea mazoezini siku kadhaa zilizopita na yuko fiti kuwavaa Jkt leo huku pia Mohamed Issa Banka na Ally Ally pia wakirejea na wako tayari kwa ajili ya mchezo huo jioni ya leo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka