Connect with us

Soka

Kiungo Mtibwa,Azam Afariki Dunia

Kiungo wa zamani wa Azam fc na Mtibwa sugar Ibrahim Rajabu Jeba amefariki dunia akiwa visiwani  Zanzibar alikokua akiichezea timu ya Chuoni fc ya visiwani humo.

Jeba aliyewahi kuichezea Azam fc,Mtibwa sugar na timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) amefariki akiwa visiwani humo baada ya kuugua na kulazwa katika hospitali ya Mnazi mmoja iliyopo visiwani humo.

Kiungo huyo enzi za uhai wake alisifika kwa soka la uhakika akitumia akili na nguvu kiasi cha kuwa tishio kwa viungo wengi nchini waliokua wakikutana nae uwanjani.

Timu ya chuoni fc anayoichezea kiungo huyo imethibitisha kifo cha mchezaji huyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka