Connect with us

Masumbwi

Ndondi Kenya Wang’ara Mashindano ya Madola

Mabondia watatu kutoka nchini Kenya wameng’ara katika mashindano ya madola yanayoendelea mjini Rabat nchini Morrocco baada ya mabondia hao kushinda mapambano yao na kufuzu nusu fainali.

Boniface Mogunde alimpiga Goma Naftar Afonso wa Angola kwa pointi hivyo atakutana na Osoba Abdul katika nusu fainali ya kwanza ya michuano hiyo na akishinda atakutana na mshindi kati ya Clair Merve wa Mauritius au  Kapenga Nsaka Idriss wa Jamhuri ya watu wa  Congo.

Elly Ajowi heavyweight (91kg) alimpiga  Mnigeria Franklin Arinze Chukwidi 3-1 na anatajiwa kukutana na Moussa Youssef  wa Misri au Muarijeria Benchabla Abdelhadif.

Fredrick Ramogi bondia wa uzito wa juu (over 91kg) alimpiga Mohammed Firise wa Morocco katika raundi ya kwanza na anatarajia kukutana na Tshikera Jeamie Kibembi kesho katika raundi ya kwanza na akishinda atakutana na mshindi kati ya  Mmisri Havez Yousry na Mnijeria Adebayo Solomon Imoleayo.

Chama cha ndondi nchini humo kimewapongeza mabondia hao na kuwataka wengine kufata nyayo zao baada ya kujihakikishia kurudi na medali.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Masumbwi